NDAYIRAJIGE ACHUKUA MIKOBA YA MINZIRO KMC
Ettiene Ndayirajige ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Ndayirajige alishindwa kumaliza msimu akiwa na timu ya Mbao FC kutokana na kushindwana baadhi ya mambo ambapo sasa anachukua nafasi ya Fred Minziro amabye atapangiwa majukumu mengine.
Raia huyo wa Burundi alifanya vizuri zaidi katika msimu wake wa kwanza 2016/17 na timu hiyo kutoka jijini Mwanza baada ya kuisaidia kuingia fainali ya kombe la FA.
Meya ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amemtambulisha kocha huyo mbele ya Waandishi wa Habari akiwa na matumaini makubwa ya kuivusha kutoka ilipo kwa sasa.
"Leo nimewaita waandishi wa habari lengo kubwa likiwa ni kumtambulisha kocha wetu mpya Ettiene Ndayirajige kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2018/19 na tumesaini mkataba wa mwaka mmoja," alisema Mstahiki Meya.
Post a Comment