SIMBA YAWAONGEZA SALAMBA, MO RASHID SPORTPESA SUPER CUP


Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba imewaongeza wachezaji wake wapya iliyowasajili Adam Salamba na Mohammed Rashid katika michuano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Jumapili nchini Kenya.

Simba iliondoka jana na kikosi cha wachezaji 18 wakiwa na nafasi ya kuongeza wawili kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo zinavyotaka.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Manara ambaye ameongozana na timu amesema wameongeza washambuliaji hao ili kuendelea kuwazoea wachezaji wenzao.

Wekundu hao waliondoka jana wakiwa pia na kiungo wao mpya mshambuliaji Marcel Kaheza waliomsajili toka Majimaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa ligi.

"Tuwaongeza washambualiaji wetu wapya Salamba na Mo Rashid kwa ajili ya michuano ya SportPesa ambapo sisi tutaanza kucheza Jumatatu," alisema Manara.

Salamba alijiunga na Simba akitokea Lipuli FC wakati Mo Rashid akitokea Tanzania Prisons.

No comments