TUNAFAHAMU UWEZO WA WAPINZANI WETU, LAKINI USHINDI NI LAZIMA KESHO DHIDI YA SHIPOLOPOLO - KOCHA WA TWIGA STARS, EDNA LEMA
Timu ya Taifa ya Soka la wanawake Tanzania “Twiga Stars” kesho
inashuka Dimba la Uwanja wa Taifa kupambana na Zambia “SHEPOLOPOLO”
ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kuwania kushiriki Fainali za Mataifa ya
Afrika “AFCON” zinakazofanyika mwaka huu nchini Ghana.
Kocha wa Timu ya Twiga Stars Edna Lema amesema, watakuwa na mchezo wenye ushindani mkubwa kwani wanauzoefu na wapinzani wao ambao walishakutana mara Tatu wakifungwa na wakishinda huku akiongeza kuwa kikosi chake kipo imara kutokana na maboresho waliyoyafanya kwa kuongeza wachezaji vijana.
“Kikubwa tumejiandaa kesho kwaajili yakushinda japo tunajua mchezo utakuwa mgumu kwasababu tulishawahi kukutana na Zambia kwahiyo naamini kutakuwa na ushindani wa hali ya juu, ” amesema.
“Kikosi kinamabadiliko kwani kunawachezaji waliona umri chini ya miaka 20 ambao tumewapandisha na wale wadogo ambao tumewachukua wachache, hivyo tunaamini wachezaji wote kwaujumla watatupa matokeo mazuri katika mchezo wa kesho, ” amesema.
Edna ameongeza kwau wanawaheshimu Zambia kwasababu wanatimu nzuri na waliwaona katika mashindano ya COSAFA ambayo wao hawakushiriki na wanatimu bora Afrika ambayo imeshiriki mashindano mengi ya Afrika lakini wanakutana na Timu bora pia ambayo ni Twiga Stars hivyo wanaamini watashinda.
Kwaupande wake Kocha Shepolopolo Carol Daka amesema, kila mchezaji amejipanga kwaajili ya mchezo huo na hana majeruhi yoyote hivyo wamewekeza nguvu zao zote katika mchezo wa kesho waajili ya ushindi.
“Kikosi changu kipo tayari kwaajili ya kupambana, hali ya hewa tuliyokutana nayo haijatushangaza sana kwani tunajua hiki ni kipindi cha mvua hivyo tumejipanga kupambana na hali yoyote tutakayokutana nayo na tunaamini tutapata ushindi”

Post a Comment