KOCHA MBAO FC ASEMA SASA KUFUNGWA BASI, KIYOMBO AKANUSHA KUZIKAMIA TIMU KUBWA LIGI KUU
Kocha
wa Timu ya Mbao FC ya Jijini Mwanza, Mrundi Ettiene
Ndayiragije
amesema, ushindani wa Ligi kwa msimu huu unatokana na kila timu
kufanya usajili wa wachezaji wazuri na kikosi chake pia kipo vizuri
na kimejipanga vizuri kwaajili ya kushinda michezo yote iliyombele
yao hususani dhidi ya Simba SC utakaopigwa Jumatatu ya Februari 26
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
“Wachezaji
wote wapo salama na wapo tayari kwaajili ya mchezo dhidi ya Simba SC,
watu wengi wamekuwa wakisema kuwa tunapokutana an Simba au Yanga huwa
tunacheza kwa nguvu ili tushinde lakini sio kweli ni hali tu ya
mchezo na sisi tumejiandaa kwaajili ya Ligi a sio wkaajili ay timu
moja pekee, ” amesema.
“Kitu nilichogundua msimu huu ni kwamba timu nyingi zimesajili vijana wazuri a wenye uwezo hivyo wanaendelea kujitoa na kujitua na imesababisha ushindani ambayo ni hali nzuri kwani tumekuwa a Ligi nzuri na yenye ushindani wa hali ya juu, ” amesema.
Naye Mshambuliaji Nyota wa Mbao FC Habib Kiyombo amesema, wanaamini mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa ya ushindani kutokana na Simba SC kutafuta matokeo mazuri ili kujiimarisha zaidi kileleni lakini kwa upande wao wakiwa ni wachezaji wamejipanga kwaajili ya kujiondoa katika hatari na kubaki salama katika Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mrundi
huyo amesema, hali ya ushindani inazidi kuwapa nguvu ya kuzidi
kupambana na hata uwiano wa pointi katika msimamo wa Ligi unaonyesha
ni jinsi gani kila timu imejiandaa lakini kwa upande wao hawatakubali
kupoteza japo wanakutana na timu ambayo inaonyesha ushindani wa hali
ya juu na pia ni kinara katika Ligi.
“Kitu nilichogundua msimu huu ni kwamba timu nyingi zimesajili vijana wazuri a wenye uwezo hivyo wanaendelea kujitoa na kujitua na imesababisha ushindani ambayo ni hali nzuri kwani tumekuwa a Ligi nzuri na yenye ushindani wa hali ya juu, ” amesema.
Naye Mshambuliaji Nyota wa Mbao FC Habib Kiyombo amesema, wanaamini mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa ya ushindani kutokana na Simba SC kutafuta matokeo mazuri ili kujiimarisha zaidi kileleni lakini kwa upande wao wakiwa ni wachezaji wamejipanga kwaajili ya kujiondoa katika hatari na kubaki salama katika Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
“Tupo
katika maandalizi mazuri na tunahitaji matokeo mazuri katika mchezo
dhidi ya Simba na tunajituma kwa kila mchezo ili kuhakikisha
tunajikwamua kutoka hapa tulipo katika simamo wa Ligi ili tuweze
kupanda na kuwa katika nafasi nzuri kwani hakuna timu inayokubali
kushuka kwenye Ligi kuu, ” amesema.
Kiyomo
amemalizia kwa kusema kuwa bado mechi ni nyingi na lengo leo ni
kutokushuka kwenye ligi hivyo bado wanapambana na wanahitaji sapoti
ya mashabiki ili waendelee kufanya vizuri zaidi.
Kikosi cha Mbao FC
Mshambuliaji nyota wa Mbao FC, Habib Kiyombo
Post a Comment