WAFAHAMU WAAMUZI WA TANZANIA WALIOTEULIWA KUCHEZESHA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA
Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa
Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi
18,2018 Madagascar.
Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii
atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli
Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa
Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis
Blaze Madeleine
Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi
ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club
Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini
utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia
mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec
Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy
Mwanawasa uliopo Ndola.
Post a Comment