SINA HAJA YA KUWAJUA KWASABABU SIWAHOFII WAPINZANI WANGU, NAWAAMINI WACHEZAJI WANGU - KOCHA WA NGORONGORO HEROES, AMY NINJE
Kocha wa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania
walionaumri Chini ya Miaka 20 “Ngorongoro Heroes” amesema, haofii
chochote katika mchezo wa kesho dhidi ya DR Congo kwani anaimani na
kikosi chake katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kushiriki
Michuano ya AFCON ya Vijana.
Akizungumza an waandishi wa habari hii leo, Kocha wa Ngorongoro Heroes Amy Ninje amesema, Kila mchezaji anajua ni nini cha kufanya katika mchezo huo na lengo ni kumaliza mchezohuo hapahapa nyumbani kabla ya mchezo wa marudiano huku akiwataka watanzania pia kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuwapa sapoti.
“Sina majeruhi katika kikosi cha wachezaji 30 na kutakuwa na mazoezi ya mwisho leo jioni kuangalia timu gani itaanza, Morali lwa wachezaji ipo ya hali ya juu na kwa hizi wiki mbili ambazo nimepata nafasi ya kufanya mazoezi na vijana nimeona kwamba wanahamu ya kuendelea kujifunza sasa mimi kila siku nakuja na majukumu mapya na ninawasaidia kwaajili ya kujijenga kuwa wachezaji bora hapo baadaye, ” amesema.
“Sinahaja ya kuwajua zaidi wapinzani wangu kabla ya mchezo kwani sihofii chochote na kesho ndio nitawajua vizuri, ” amesema.
Kocha Ninje amesema, kwenye soka hakuna kitu kizuri kama uzoefu hivyo kutokana na kikosi chake kucheza mechi takribani 30 walipokuwa katika kikosi cha U17 hivyo kwake ni faida kwani anaamini wachezaji hao wanauzoefu mzuri japo hawakuwa pamoja kwa muda mrefu lakini kambi waliyokuwa nayo kwa kipindi hiki imeweza kuwaweka sawa kwaajili ya mchezo huo.
Kwaupande wake Kocha wa DR Congo Jean Claude Mukanya amesema, wachezaji wote aliowasili nao wapo imara japo kunamapungufu ndani ya kikosi lakini hayatamzuia kuweza kufanya vizuri katika mchezo huo.
“Kikosi changu kipo imara kwaajili ya kupambana hapo kesho, japo ninamajeruhi wengi ambao nafasi zao zimechukuliwa na wachezaji wapya ndani ya kikosi lakini naamini watapambana na nia yetu kwa ujumla ni kupata matokeo mazuri japo tunajua tupo Uwanja wa ugenini, ” amesema.

Kocha wa Ngorongoro Heroes, Amy Ninje |
Post a Comment