TFF YAWATAKA DODOMA FC KUWA WAVUMILIVU KUSUBIRI MAJIBU YA RUFAA YAO
Shirikisho
la Soka nchini TFF limeitaka Timu ya Dodoma FC kuwa wavumilivu katika
kusubiri majibu ya rufaa kama kweli imefuata masharti kwani walitoa
nafasi kwa timu zenye malalamiko kuweza kuyawasilisha.
Afisa habari wa TFF Mario Clifford Ndimbo amesema, kanuni walizonazo ni kutotangaza timu iliyopanda Daraja kushiriki Ligi kuu msimu ujao kabla ya saa 72 kukamilika na pia ziliwekwa taratibu za kukata rufaa na hata kupangwa siku ya kuweza kusikiliza hivyo wanasubiri taratibu zote zikamilike ili waweze kutaja timu iliyopanda rasmi kushiriki Ligi kuu kwa msimu wa mwaka 2018/19.
“Kama Dodoma FC wanasema wamekata rufaa maanayake kunataratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa katika ukataji wa rufaa na kama wametimiza maana yake baadaya hapo itapangwa siku ya kuweza kusikiliza kwasababu unapokata rufaa maana yake ni kwamba huwezi kukata leo na leo leo ikasikilizwa, hivyo kama wamekata rufaa kwa kufuata kanuni maana yake itasikilizwa, ” amesema.
Ndimbo amesema, wao wakiwa ni wasimamizi wa Ligi wametoa nafasi kwa timu zote shiriki Ligi daraja la kwanza na zilizowasilisha malalamiko kwa kuzingatia kanuni zitasikilizwa kwa kuzingatia haki na usawa na siku yoyote watatangaza pia timu zilizopanda Daraja kwa haki.
Dodoma FC ilitoa malalamiko na kudai imeshayatuma Bodi ya Ligi wakiwalalamikia wapinzani wao Toto African kumtumia mchezaji ambaye hakuwa na leseni huku Timu za Alliance Schools ya Mwanza na Biashara ya Musoma zikiwa zinaongoza kundi ikionyesha kuwa zimeshapanda daraja.

![]() |
Kikosi cha Timu ya Dodoma FC kikiwa Mazoezini |
Post a Comment