BAADA YA KUSUA SUA KWENYE LIGI KUU, SINGIDA UNITED SASA YAHAMISHIA NGUVU KWENYE FA
Klabu ya Singida United imesema nguvu na mawazo kwa sasa
wanaelekeza katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) ambapo
wataikaribisha Polisi Tanzania Jumamosi ya Februari 24lengo likiwa ni
kusonga mbele na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa
hapo baadae.
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema mashindano hayo yanaweza kuwaweka katika nafasi nzuri japo wanakutana na timu ngumu na yenye uwezo huku wakimkosa Kambale Salita mwenye kadi nyekundu lakini wanaamini watapita katika hatua ya 16 kombe la Shirikisho.
“Tunamchezo wa FA dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumamosi majira ya saa 10 jioni Uwanja wa Namfua, maandalizi yanaendelea vizuri na tumekuwa na muendelezo mzuri kwenye FA na ukiangalia kwenye mashindano haya ni njia fupi kuliko Ligi kuu na tumewekeza nguvu za kutosha kwenye FA kuhakikisha tunashinda mchezo huo, ” amesema.
Sanga amesema, kikoso chote kipo imara kwaajili ya mchezo huo hivyo anaamini kila mchezaji atapambana ili kuhakikisha timu inasonga mbele katika michuano hiyo.
Wakati huohuo Sanga amesema, mara baada ya mchezo huo watasafiri mpaka jijini Dar es salaam kwaajili ya kupambana na Azam FC katika mchezo wa Ligi kuu utakaopigwa Februari 27 ambao katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoka sare ya bao 1-1 na wamepania kuwashusha wapinzani wao hao mpaka nafasi ya Tatu huku katika mchezo huo wakiwa na kikosi kamili wakiwemo wachezaji waliokuwa majeruhi.
“Tunahistoria na Azam FC kwa sababu tulicheza mchezo wetu wa kwanza pale Dodoma na tulitoka sare walisawazisha dakika ya 92, lakini pia mzunguko huu wa pili tunakwenda kukutana na Azam FC pale Chamazi, nimchezo ambao tukishinda tunamshusha Azam FC mpaka nafasi ya nne na sisi tunapanda mpaka nafasi ya Tatu, na Azam hatamani kuona anafungwa lakini hakuna namna kwani lengo letu ni kuweza kushika nafasi tatu za juu na licha ya kwamba tumekuwa tukisua sua lakini tunahitaji kushinda Chamazi, ” amesema.
Kikosi cha Singida United

Post a Comment