MASAU BWIRE AMESEMA HAWANA SHAKA KUWA WATASALIA VPL MSIMU UJAO
Baada ya klabu ya Ruvu Shooting kuchomoza na ushindi mujarabu wa mabao 3
– 1 dhidi ya Lipuli FC msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire amesema kuwa
kwa sasa lazima kuchomoza na pointi tatu kwa kila mchezo watakao cheza.
“Hiyo ndiyo Ruvu Shooting mpira tunao cheza sasa timu yoyote lazima
iwache pointi, ushindi huu tuliutarajia na tunakuja,”amesema msemaji wa
Ruvu Masau Bwire.
“Sisi siyo watu ambao tuna kuja ila ni uwezo, Ruvu Shooting hatujafa,
hatutakufa na wala hatutarajii kufa hebu waulize Lipuli FC tulicho
mfanya.”
“Tunashukuru waamuzi walikuwa wazuri na wenye viwango vya hali ya juu
vya kutafsiri kanuni za ligi kuu na hakuna waliyo walalamikia hata
baada ya kumalizika kwa mchezo.”
Kufuatia matokeo hayo ya ushindi mnono wa mabao 3 – 1 dhidi ya Lipuli
FC klabu hiyo ya Ruvu Shooting sasa inakuwa nafasi ya saba katika
msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 20.
Michezo mingine iliyopigwa hapo jana na msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa sasa.
Post a Comment