MWAKYEMBE AMERIDHISHIWA NA SIMBA NA YANGA KATIKA HILI.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
ameridhishwa na kiwango cha Simba jana katika michuano ya kimataifa na
kukiri kuwa kwasasa Tanzania sio kichwa cha Mwendawazimu tena.
Akiongea mbele ya wanahabari Mwakyembe alieleza furaha yake kuona
timu mbili zinazoiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya kimataifa
Yanga SC na Simba SC zikiibuka na ushindi katika mechi zake za kwamza.
''Kama kiwango cha mpira wa miguu Tanzania kitakuwa hiki, basi sisi
sio tena kichwa cha Mwendawazimu kwasababu kiwango cha timu hizi
kinaonesha kweli timu zimekuwa kambini na zina walimu wazuri, sisi ni
kichwa cha Muungwana'', amesema.
Yanga inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika
ambapo katika mchezo wake wa hatua ya awali jumamosi iliyopita iliibuka
na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.
Simba wenyewe wanaiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la
shirikisho barani Afrika ambapo jana imeibuka na ushindi wa mabao 4-0
dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti.
Post a Comment