WENGER HANA MPANGO WA KUONDOKA ARSENAL KABISA
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema katika maswali yanayomfurahisha
ni yale yanayohusu hatima yake ndani ya timu hiyo ambayo ameifundisha
tangu mwaka 1996.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kama kuna kitu hakimuwazishi ni
nafasi yake ndani ya Arsenal licha ya kupoteza mechi sita kati ya 12
ndani ya mwaaa 2018 ndio mana huwa anafurahia maswali yanayouliza hatima
yake.
''Siwazii mkataba kwasasa zaidi nafikiria namna ya kuifanya timu
iwaze mchezo wa kesho'', amesema Wenger kuelekea mchezo wa EPL kesho
dhidi ya vinara Manchester City.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 alisaini mkataba mpya wa miaka
miwili mwezi Mei 2017 licha ya kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya
Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 20.
Post a Comment