BMT YASITISHA UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA NGUMI NCHINI.
Baraza la Michezo nchini (BMT)
limesitisha uchaguzi wa Shirikisho la ngumi nchini (BFT) uliotakiwa kufanyika
Jumamosi ya Ferbruari 24 mjini Dodoma mara baada ya kukuta kasoro ndani ya
katiba ya shirikisho hilo.
Afisa habari wa BMT amesema mara
baada ya kukutana na kasoro hizo, Katibu Mkuu Mohamed Kiganja aliunda kamati
yenye wajumbe sita ambao wamepewa majukumu ya kuhakikisha wanarekebisha katiba
ikishirikiana na Serikali ndani ya miezi mitatu.
"Kamati hiyo imepewa majukumu
yakurekebisha katika ili iweze kwenda sawa na shirikisho ikiwa ni pamoja na
kuwa na dhumuni, na ndani ya miezi hii mitatu wahakikishe wanaandaa
mkutano mkuu wa uchaguzi na katika mkutano huo wahakikishe kwamba ili
kuwapunguzia gharama wanachana ambao ni wapiga kura wahakikishe wanawapunguzia
mzigo kwa kushirikiana na Baraza, watafute pesa kwaajili ya kuwasaidia katika
uchaguzi utakaofanyika hapo baadae, " amesema.
Najaha amesema, katika kamati hiyo
iliyochini ya Rais wa BFT Mutta Rwakatare imetakiwa kuyafanyia kazi Yale yote
waliyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kulenga katika katiba kunakuwa na kanuni za
uchaguzi, ufundi na utawala ili kuhakikisha shirikisho hilo linasonga mbele.
Najaha amemaliza kwa kutoa wito kwa
Vyama na maahirikisho kuhakikisha katiba zao zinakuwa na vigezo na kuwa na
mazoea ya kupeleka katiba kwa msajili ili katiba ziweze kufanyiwa marekebisho
pale panapostahili.
Post a Comment