BARCELONA WAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LALIGA WAIPOTEZA ATLETICO MADRID CAMP NOU.
Klabu ya Barcelona imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu
ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa mzunguuko wa 27 wa La Liga.
Goli la Barcelona limefungwa na mshambuliaji wake Lionel Messi kwa
mpira wa adhabu ya moja kwa moja ambapo hadi dakika 90 zinamalizika goli
hilo lilidumu.
Kwa matokeo hayo Barca inakuwa na alama 69 ikifuatiwa na Atletico
yenye alama 61 huku Madrid wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La
Liga kwa alama 54.
Post a Comment