SIMBA KUTUMIA SIKU HIZI KWAAJILI YA KUIWINDA AL MASRY!!!
Baada ya kupewa mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba hatimaye jioni
ya leo kimeanza rasmi maandalizi ya mchezo wake wa kwanza Kombe la
Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.
Kikosi hicho chini ya kocha Mfaransa Pierre Lechantre kilipewa
mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Stand
United uliomalizika kwa sare ya 3-3 ijumaa jioni.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa timu hiyo ipo kambini tayari kwa
maandalizi ya mchezo huo ikianza na mazoezi ya jioni leo na itafanya
hivyo hadi jumanne jioni kisha jumatano kushuka kwenye uwanja wa taifa
kukipiga na Wamisri.
''Kikosi cha Simba kimeingia kambini tayari kujiandaa na mchezo dhidi
ya Al Masry utakaochezwa siku ya Jumatano saa 12:00 jioni'', imeeleza
sehemu ya taarifa.
Simba imetinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kushinda kwa
jumla ya mbao 5-0 kwenye mchezo wa hatua ya awali dhidi ya timu ya
Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.
Post a Comment