HIKI NDICHO KINACHOSUBIRIWA NA BMT KABLA YA KUTOA TAMKO KUHUSU KUFUNGIWA KWA MAKAMU WA RAIS WA TFF KUTOKUJIHUSISHA NA SOKA
Mara
baada ya Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF)
kumfungia maisha kutokujihusisha na masuala ya Soka aliyekuwa Makamu
wake Michael Wambura, Baraza la Michezo nchini (BMT) limesema, bado
halijapokea barua kutoka kwa shirikikisho hilo kuhusiana na maamuzi
hayo.
Katibu
Mkuu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema, kwa sasa ni mapema mno
kulizungumzia suala hilo kwani mpaka sasa hawajapewa chochote kile
zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
“Mpaka
sasa sisi kama serikali hatujapewa chochote kuhusiana na suala hilo
kwahiyo sio rahisi kuzungumzia kitu ambacho unakisikia kwenye
mitandao na kwenye vyombo vya habari hivyo hatuwezi kutoa maelekezo
yoyote, ” amesema.
Kiganja
amesema, suala lililotokea TFF halina pande moja hivyo wanasubiri TFF
waieleze serikali walipoanzia mpaka walipoishia na hata Wambura pia
ambapo mara baada ya kupata pande zote mbili ndipo watatoa tamko kama
itatakiwa.
Kiganja
amesema, jambo lililotokea ni kubwa na halipaswi kukaliwa kimya na
limeshtua Watanzania, wadau wa Soka na hata nchi kwa ujumla.
Wambura
amefungiwa kutokujihushisha na soka kwa makosa matatu ya kupokea
fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya
TFF.
![]()
| |
Post a Comment