ROGER FEDERER AMEPIGA MKOREA NA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI INDIAN WELLS.

Mchezaji tennis, Roger Federer amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Indian Wells na kuendelea kulinda heshima yake ya kuwa namba moja kwa viwango vya ubora duniani.


Federer amefanikiwa kutinga hatua hiyo siku ya hapo jana siku ya Alhamisi usiku baada ya kumshinda Mkorea Kusini, Chung Hyeon kwa jumla ya seti 7-5 6-1.

Mchezaji huyo mwenye umri mkubwa zaidi katika tennis anatarajia kukutana na Borna Coric, ambaye amemfunga Kevin Anderson kwa seti 2-6 6-4 7-6.

Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.


No comments