MFAHAMU KIPA WA YANGA AMBAYE ANAMPANGO WA KUTIMKA KATIKA KIKOSI HICHO.
Mlinda mlango namba tatu wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania
Bara Yanga, Beno Kakolanya, huenda msimu ujao akahamia timu ya JKT
Tanzania iliyorejea ligi kuu msimu huu.
Meneja wa mchezaji huyo Suleiman Haroub amesema kwamba hadi sasa
amepokea ofa nne zikiwemo za timu za JKT Tanzania na KMC ambazo zote
zitashiriki ligi kuu msimu ujao.
Kakolanya amekosa namba mbele ya walinda milango Youthe Rostand na
Ramadhani Kabwili huku pia mkataba wake ukiwa unaelekea kumalizika hivyo
meneja wake amesisitiza kuwa bado wanaisikiliza Yanga kabla ya kutazama
ofa nyingine.
"Ni kweli hizo ofa zipo tumezipokea na wamekuja tumezungumza nao
lakini bado tunawasikiliza Yanga ambao hadi sasa wanamkataba naye lakini
wapo kimya'', amesema Haroub.
Golikipa huyo kwasasa kaachwa nchini na kikosi cha Yanga
kilichosafiri kwenda Botswana kwaajili ya mchezo wa marudiano ligi ya
Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers. Mchezo huo utapigwa kesho
jioni na katika mchezo wa kwanza Township ilishinda 2-1.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment