SIMBA KATIKA MAWINDO MAKALI YA KUPATA USHINDI DHIDI YA AL MASRY UGENINI JE ITAWEZEKANA.
Kikosi cha Simba hii leo kimeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa
Boko Veterani jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake
dhidi ya Al Masry mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika CAF
utakaopigwa Machi 17, 2018 nchini Misri.
Mchezo wa awali uliyopigwa hapa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita,
timu hizi mbili zilitoka sare ya kufungana mabao 2 – 2 na hivyo
watalazimika kuchomoka na ushindi ili kujihakikishia wanasonga mbele.
Post a Comment