MOISE KATUMBI AMEANZISHA CHAMA CHAKE CHA SIASA AKIWA AFRIKA KUSINI
Rais wa klabu ya
TP Mazembe ya katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi amejitosa
kwenye ulingo wa siasa, anazindua chama chake akiwa Afrika Kusini.
Katumbi ni
kiongozi wa upinzani ambaye yupo uhamishoni kutoka DR Congo baada ya kutengana
na Rais Joseph Kabila.
Katumbi ambaye
amewahi kuwa Gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo Katanga alijiuzulu na
kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duniani.
Moise Katumbi ni
kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na
ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo na anayetarajiwa kumpa rais Kabila
ushindani mkali endapo atawania tena.
Alitangaza kutaka
kuwania urais mwaka 2016, kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.
Katumbi aliondoka
DRC Mwezi Mei mwaka 2016 na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu
punde tu aliposhutumiwa kuwaajiri wapiganaji. Baada ya hapo alihukumiwa bila
yeye kuwepo kwa kuuza maeneo kinyume cha sheria na kupatiwa kifungo cha miaka 3
jela.
Anakanusha tuhuma
hizo na amewahi kusema kuwa bado anataka kuwania urais katika uchaguzi
utakaofuata. Bw Katumbi pia ni ya soka maarufu ya TP Mazembe.
Post a Comment