EMILY MUGETA AREJEA RASMI UWANJANI NA KUTUPIA MOJA NYAVUNI

Mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini ujerumani Emily Mugeta hatimaye amerejea rasmi dimbani baada ya kukaa nje kwa mwaka mzima akiuguza majeraha.

Akizungumza na TikTakTz Mugeta amesema 'Baada ya kukaa muda mrefu nje nikiuguza jeraha la bega hatimaye jana nimerudi rasmi uwanjani baada ya mwaka mmoja na week mbili,jana nimeanza kucheza rasmi mechi huku nikiwa na timu ya pili ya VfB Eppingen 2 kucheza kwangu mechi nikiwa na Kikosi cha pili ni kwaajili ya kujenga matchfitness kwa maana nilikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana hivyo lazima nianzie Kikosi cha pili ndo nirudi kikosi cha kwanza mala ntakapokuwa Fiti kwa asilimia 100'Amesema Mugeta.

Katika mchezo huo wa jana Mugeta aliweza kufunga bao moja na kutoa assist mbili.Hakika hii ni taarifa nzuri kwa mchezaji huyu.Uongozi mzima wa Tiktaktz pamoja na Mugeta soccar academy unamtakia kila la kheri katika harakati zake.

No comments