SERENGETI BOYS KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA DHIDI YA UGANDA JUMAPILI, MICHUANO YA CECAFA U17 BURUNDI

Kikosi cha wachezaji 20 cha timu ya Taifa ya Soka la vijana walio na umri chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" kilichoondoka hapo jana kuelekea nchini Burundi kwaajili ya michuano ya CECAFA inayoanza kutimua vumbi hapo kesho, Jumapili kinatarajia kutupa Karata yake ya kwanza dhidi ya Uganda.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Clifford Ndimbo amesema, maandalizi bora waliyoyatoa kwa wachezaji wanaounda kikosi hicho ikiwemo mechi za kirafiki wanaamini wataipeperusha vema bendera ya Tanzania katika michuano hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya AFCON U 17 itakayofanyika mwakani Tanzania ikiwa ni nchi mwenyeji.

"Kikosi kimeondoka vizuri kikiwa na imani kubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanaanza kesho lakini Tanzania itatupa karata yake ya kwanza siku ya Jumapili, " amesema. 

Ndimbo amesema, waliwaandalia mazingira ya kwenda kufanya vizuri vijana hao kwa kwa na mechi mbalimbalï za kirafiki dhidi ya vijana wenye umri sawa na wao ambapo waliweza kuonyesha kiwango kizuri.
Michuano ya CECAFA inashirikisha timu nane zikiwa katika makundi ambapo kundi A kunatimu za Somalie, Ethiopia, Burundi na Kenya huku kundi B kukiwa na timu za Tanzania, Sudan, Zanzibar na Uganda.

Serengeti Boys

No comments