AZAM KWENDA 'PRE SEASON' UGANDA
Kikosi cha Azam FC kitaenda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2018/19 'Pre Season' nchini Uganda kama walivyofanya mwaka uliopita.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu Wana lamba lamba hao walienda kufanya ziara nchini Uganda na kucheza mechi kadhaa za kirafiki.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema baada ya wachezaji kurejea kutoka likizo mwezi Julai wataenda kuweka kambi Uganda kujiandaa na msimu mpya wa ligi.
"Tutaenda kuweka kambi Uganda kujiandaa na msimu mpya wa ligi kama tulivyofanya mwaka jana kwa sasa wachezaji wapo likizo," alisema Jaffer.
Jaffer ameongeza kuwa wachezaji wao wa kigeni walianza kuondoka jana usiku baada ya mechi ya Yanga na leo atamalizia mlinzi Yakub Mohammed.
Azam imefanikiwa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga.
Post a Comment