KONDO: UBABAISHAJI UMEISHUSHA DARAJA MAJIMAJI


Kocha mkuu wa Majimaji, Habib Kondo amefunguka kuwa moja ya sababu iliyofanya timu hiyo kushuka daraja ni ubabaishaji wa viongozi wao.

Kondo amesema migogoro ilianza tangu kwenye usajili ambapo wachezaji walisaini mikataba huku wakiwa hawajapewa pesa zao kamili kitu ambacho kilishusha morali.

Kocha huyo aliongeza kuwa hata yeye mwenyewe anaudai uongozi huo pesa za malimbikizo ya mishahara yake.

"Kwakweli tulistahili kushuka daraja, timu ilikuwa ina ubaishaji mwingi wachezaji hawakupata stahiki zao kwa wakati ndio maana imeshuka daraja," alisema Kondo.

Wakati huo huo kocha huyo ametangaza kutoendelea kufanya nayo kazi msimu ujao katika ligi daraja la kwanza.

No comments