SIMBA KUFANYA BONGE LA 'SUPRISE' KABLA YA KWENDA KENYA

Uongozi wa klabu ya Simba umeahidi kufanya usajili mkubwa utakaotikisa nchi kabla ya kwenda Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup wiki ijayo.

Tayari mabingwa hao wa ligi kuu wamekamilisha usajili wa washambuliaji wawili Marcel Kaheza kutoka Majimaji na Adam Salamba wa Lipuli FC lakini wameahidi kuongeza makali.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema watafanya usajili utakao tikisa nchi na watasafiri na mchezaji huyo kushiriki michuano ya SportPesa huko Kenya.

Manara amesema wanahitaji kufanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa Afrika hivyo wanaandaa kikosi madhubuti ili kufanya vizuri.

"Tutafanya usajili ambao utashtua nchi kabla ya kwenda Kenya kushiriki michuano ya SportPesa wiki ijayo, tunataka kuandaa imara kikosi kwa ajili ya msimu ujao.

"Hao wakina Kaheza na Salamba ni trela picha linakuja siku chache kutoka sasa litakuwa bonge la Surprise," alisema Manara.

No comments