SINGIDA KUCHOMOA STRAIKA WA PRISONS
Singida United naendelea kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi na wapo mbioni kukamilisha usajili mshambuliaji Eliuter Mpepo kutoka Tanzania Prisons.
Mchana wa leo Singida ambayo tayari imeondokewa na kocha wao mkuu Mholanzi, Hans van Pluijm aliyejiunga na Azam FC wamewatambulisha wachezaji watatu, wawili wa kigeni na mmoja wa ndani kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao cha msimu ujao.
Rafiki wa karibu na mshambuliaji huyo ameuambia mtandao huu kuwa kila kitu kimekaa sawa kinachosubiriwa ni muda tu wakutiliana saini.
"Mpepo yuko mbioni kujiunga na Singida, wamefanya mazungumzo na wameafikiana na alikuwa nao jana na leo amerejea Dar es Salaam muda si mrefu atatangazwa," alisema rafiki huyo.
Mpepo anakuwa mshambuliaji wa pili kutoka nchini kujiunga na Singida baada ya Tibar John kutoka Ndanda kutambulishwa leo huko jijini Arusha.
Post a Comment