YONDANI AZIDI KUIPASUA KICHWA YANGA


Mlinzi wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni ameichanganya timu hiyo kwa kushindwa kupatikana kwenye simu huku akiwa hajulikani alipo.

Yondani amekuwa muhimili mkubwa katika idara ya ulinzi ya Yanga ni miongoni mwa walinzi wa Tanzania waliodumu kwenye kiwango bora kwa muda mrefu.

Nahodha huyo msaidizi anahusishwa na kutaka kurejea timu yake ya zamani ya Simba ambayo inataka kuibomoa Yanga huku pia Azam FC wakihusishwa nae.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema leo watakutana na wachezaji wote kwa ajili ya kujadiliana kuhusu michuano ya SportPesa Super Cup ambapo kikosi kitaondoka kesho kuelekea Nairobi hivyo kila kitu kitajulikana.

"Yondani mkataba wake unaelekea mwishoni na leo tutakuna na wachezaji kwakua kesho timu inaenda Kenya kwenye michuano ya SportPesa.

"Kuhusu kutopatikana kwenye simu inawezekana labda simu yake ina matatizo ila leo ndio kila kitu kitajulikana baada ya kukutana," alisema Mkwasa.

Tayari timu mbalimbali zimeanza kufanya usajili kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kwa msimu mpya wa ligi 2018/19.

No comments