TFF YATAJA VIINGILIO VYA FAINALI YA FA
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa fainali ya kombe la FA kati ya Singida United dhidi ya Mtibwa itakayofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumamosi.
Viingilio hivyo vitakuwa kama ifuatavyo mzunguko sh 1000, mageti A na B itakuwa sh 2000 wakati VIP A itakuwa sh 10,000.
Msemaji wa Shirikisho hilo Clifford Ndimbo ametangaza viingilio hivyo mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo Karume Dar es Salaam muda mfupi uliopita.
Bingwa wa michuano hiyo atapata kikombe pamoja kitita cha sh milioni 50 mshindi wa pili atapata sh milioni 10 ambapo msimu uliopita hakukuwa na zawadi.
Mbali na zawadi hizo kutakuwa pia tuzo ya mchezaji bora wa fainali, mchezaji bora wa michuano, kipa bora na mfungaji bora.
"Tumeamua kuweka viingilio vya bei ya chini ili kuiwawezesha mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi," alisema Ndimbo.
Simba ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Mbao FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Post a Comment