FRED KUTAMBULISHWA MAN UNITED SAA 24 ZIJAZO


Manchester United inatarajia kumtangaza kiungo Fred Rodrigues ndani ya saa 24 baada ya Mbrazil huyo kufuzu vipimo vya afya kwa mujibu wa mpiga picha wa Mashetani hao Craig Norwood kupitia mtandao wa Twitter.

Fred 25, alikuwa akihusishwa pia kutaka kujiunga na Manchester City katika dirisha la usajili la mwezi Januari kabla ya Mashetani hao kuingilia kati na kumchukua.

Kiungo huyo amejiunga na United akitokea Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwa ada ya pauni 53 milioni.

Fred anaenda kucheza sambamba na viungo Nemanja Matic na Paul Pogba katika eneo la kati la kiungo la United.

Fred anatarajiwa kuimarisha idara ya kiungo cha kocha Jose Mourinho kutokana na kasi yake pamoja na uwezo wa kukaba na kushambulia.


No comments