MZEE AKILIMALI: MABADILIKO YANGA NI LAZIMA


Katibu wa baraza la wazee wa timu ya Yanga,  Mzee Ibrahim Akilimali amesema kwa sasa hakuna mjadala kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kutoka umiliki wa wanachama kwenda katika mfumo wa hisa.

Kesho Yanga watafanya mkutano mkuu wa wanachama ambapo moja ya ajenda itakuwa ni mabadiliko ya uendeshaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda mfumo wa hisa.

Mzee Akilimali ambaye amekuwa akionekana kama hapendi maendeleo ya klabu hiyo kwa kupinga mambo kadhaa amekubali kwa moyo mmoja timu hiyo kwenda katika mfumo wa hisa.

"Kwa sasa hakuna kitu kingine zaidi ya kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa timu hii. Katiba yetu inaruhusu jambo hili kufanyika.

"Tulitakiwa tungie katika mfumo huu tangu mwaka 2006 lakini ikashindikana ila safari hii mabadiliko hayakwepeki. Katiba yetu inaonyesha mwekezaji atachukua hisa asilimia 49 wanachama tunabaki na 51," alisema Mzee Akilimali.

Tayari watani wao wa jadi Simba wapo katika hatua ya mwisho kuelekea kubadili mfumo wa uendeshaji kwenda kwenye hisa wakati Mbeya City wakiwa tayari wameingia.

No comments