RASMI NGOMA NJE YA UWANJA WIKI TISA




Mshambuliaji mpya wa timu ya Azam, Donald Ngoma ataendelea kukaa nje ya uwanja kwa wiki tisa kutoka leo kuuguza jeraha la uvimbe wa goti linalomkabili.

Ngoma alipata alipata jeraha hilo miezi saba iliyopita akiwa na timu yake ya zamani ya Yanga ambapo alishindwa kupata matibabu kwa wakati.

Daktari wa timu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa ndiye aliyesafiri na mshambuliaji huyo kwenda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo katika hodpitali ya St Vincent Parrot ili kujua ukubwa wa jeraha hilo.

Dk.Mwankemwa amesema Ngoma alikuwa ana uvimbe kwenye goti la kulia ambapo baada ya vipimo imeonekana alikuwa amechanika kidogo ingawa katika matibabu yake hatafanyiwa upasuaji.

"Tumerudi asubuhi ya leo kutoka Afrika Kusini vipimo vinaonyesha Ngoma alikuwa ana uvimbe kwenye goti la kulia na ili kupona hadi kurejea katika hali yake ya kawaida atapaswa kukaa nje ya uwanja wiki tisa kuanzia Sada," alisema Dk. Mwankemwa.

Ngoma anatarajia kuondoka Jumanne kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mapumziko akiendelea kuuguza jeraha lake.

No comments