NI GOR MAHIA DHIDI YA SIMBA FAINALI SPORTPESA
Miamba ya soka Tanzania timu ya Simba itakutana na Gor Mahia katika fainali ya michuano SportPesa Super Cup itayofanyika siku ya Jumapili.
Gor imekuwa timu ya pili kuingia fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya pili.
Katika mchezo wa kwanza ulioanza saa 7 alasiri Simba iliibuka na ushindi wa penati 5-4 dhidi ya Kakamega Homeboyz.
Hata hivyo ladha ya mchezo huo ilipungua hasa kipindi cha kwanza kutokana na mvua kubwa kunyesha na kupelekea uwanja kujaa maji.
Mabao yote ya Gor yalifungwa na Meddy Kagere dakika za 37 na 88 na kufanisha mabingwa hao kuingia fainali.
Singida na Kakamega watacheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu siku hiyo hiyo saa 7 alasiri.
Post a Comment