MASOUD AUKUBALI MZIKI WA SALAMBA


Licha ya kucheza dakika chache katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya KK Homeboyz mshambuliaji mpya wa Simba, Adam Salamba amemvutia kocha msaidizi Masoud Djuma.

Salamba aliingia uwanjani dakika ya 78 kuchukua nafasi ya mshambuliaji kinda Rashid Juma na kuwasumbua walinzi wa Kakamega hali iliyomfurahisha kocha huyo.

Masoud amesema kuwa Salamba ni mchezaji mzuri ndio maana wamemsajili na wanatarajia atafanya vizuri akizidi kuzoea mazingira ya mabingwa hao.

Salamba alijiunga na Simba akitokea Lipuli FC muda mfupi baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kutokana na uwezo mkubwa aliyo uonyesha akiwa na Wana Paluhengo hao wa Iringa.

"Salamba ni mchezaji mzuri na ameanza vizuri, nategemea kumuona akifanya vizuri zaidi kadiri muda unavyozidi kwenda," alisema kocha Masoud.

Katika mechi mbili ilizocheza Simba katika michuano ya SportPesa inayoendelea nchini Kenya, Simba haijafunga bao katika muda wa kawaida mara zote imeshinda kwa penati.

No comments