SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA



Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika  Hospitali ya Sinza Palestina alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Sam wa Ukweli amefariki saa nane usiku wa ambapo ni siku tano tangu kufikishwa Hospitalini hapo siku ya jumamosi kwa ajili ya matibabu.

Mwili wa Marehemu umetolewa Sinza upo kwenye hospital ya rufaa ya Mwananyamala.

Sam wa Ukweli amewahi kutamba na vibao kama Sira raha, Hata kwetu wapo, Kisiki cha Mpingo na nyingine nyingi.


No comments