SIMBA YAKOSA TIKETI YA KWENDA GOODISON PARK


Timu ya Simba imeshindwa kupata tiketi ya kwenda Uingereza kucheza na Everton baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Gor Mahia katika mchezo wa fainali ya SportPesa.

Kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo bingwa atakwenda kucheza na Everton katika uwanja wa Goodison Park.

Simba ambayo haikuwa na baadhi ya nyota wake hasa wa kigeni imemaliza michuano hiyo bila kufunga bao hata moja huku wakiruhusu mawili.

Katika mchezo huo ambao Simba walizidiwa kiasi kikubwa mabao ya Gor yalifungwa na Maddie Kagere na Jacque Tuisenge kila kipindi.

Kagere ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara pili mfululizo baada ya kufunga mabao manne.

Mwaka jana pia Gor inayonolewa na Muingereza Dylan Kerr ilicheza na Everton katika uwanja wa taifa Dar es Salaam baada ya kuibuka na mabingwa wa michuano hiyo.

No comments