SINGIDA YAAMBULIA NAFASI YA TATU SPORTPESA
Singida United imeibuka mshindi wa tatu katika michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega Homeboyz kwa mikwaju ya penati 4-1.
Singida ilitoka nyuma bao moja na kusawazisha bao hilo kufuatia jitihada kubwa walizofanya vijana hao wa kocha Hemed Moroco.
Kakamega walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne kupitia kwa Wycliff Opondo baada ya walinzi wa Singida kuchelewa kuondoa hatari.
Baada ya bao hilo Singida walizinduka na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Kakamega lakini walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.
Danny Lyanga aliisawazishia Singida bao hilo kwa kichwa dakika ya 63 baada ya kupokea krosi safi upande wa kulia kutoka kwa Miraji Adam.
Penati za Singida zilifungwa na Deus Kaseke, Miraji, Shafik Batambuze na Lyanga.
Post a Comment