YANGA YAUNDA UONGOZI WA MPITO BAADA YA KUKUBALI MABADILIKO


Klabu ya Yanga imeunda kamati ya watu 12 kwa ajili ya kuiongoza timu katika kipindi hiki ambacho wamekubali kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda katika hisa.

Kupitia mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika katika bwalo la Polisi Osterbay, Yanga imepitisha mfumo ambapo Mwenyekiti wake wa zamani Yusuph Manji anapewa nafasi ya kurejea kuwa Mwekezaji.

Kamati hiyo itaongozwa na Tarimba Abbas na Makamu wake atakuwa Said Meck Saadiq.

Wajumbe wake ni Abdullah bin Kleb, Hussein Nyika, Samwel Lukumay, Yusuphed Mhandeni,  Hamad Islam na Makaga Yanga.

Wengine ni Ridhiwani Kikwete, Mashauri Lucas, Majid Suleiman na Hussein Ndama.

Wakati huo Yanga imeunda bodi mpya ya wadhamini ambayo itakuwa na wajumbe George Mkuchika, Fatuma Karume, Jaji mstaafu Mkwawa, Mzee Kitandu na Francis Kifukwe.

No comments