AUDIO:SINGIDA UNITED YAAPA KUSHIKILIA NAFASI YA TATU NA KUISHUSHA AZAM FC MPAKA NAFASI YA NNE MSIMAMO WA LIGI

 
Kuelekea katika mchezo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara utakaopigwa Jumamosi ya Machi 03 mwaka huu ukiwakutanisha Azam FC wakiwakaribisha Singida United Uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam, Singida United wamesema mchezo huo ndio utakaoamua nani ashike nafasi ya Tatu msimamo wa Ligi ikiwa ni hatua ya mzunguko wa lala salama Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema, japo wanakutana na wakongwe kuliko wao katika Ligi lakini wanauwezo wa kuwashusha mpaka nafasi ya nne na wao kushika nafasi ya Tatu kwani licha ya kutokuwa na mwenendo mzuri katika Ligi lakini wanaamini uwekezaji walioufanya ndani ya Timu ni lazima uendane na matokeo wanayoyahitaji.

Sanga amesema, Azam FC ni moja ya Timu wanayoiheshimu sana kutokana na uwezo pamoja na uwekezaji walionao katika Soka, lakini kwa upande wao wamedhamiria kuweza kushinda mchezo huo ili kuweza kujiweka katika nafasi ya Tatu na hatimaye kuweza kupanda zaidi na kufikia nafasi ya pili mpaka kumalizika kwa Ligi.

Sanga amesema, kikosi cha Singida United kimeshawasili jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo na wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri akiwemo Lubinda Mundia ambaye alikuwa ni majeruhi lakini kwa sasa yupo vizuri kiafya na anaendelea na mazoezi ndani ya kikosi hicho.

Sanga amesema wachezaji wote wapo sawa kisaikolojia pia kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo. 

Msikilize Sanga hapa chini:         



Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu, Azam FC iliilazimisha sare ya bao 1-1 Singida United katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma mabao yaliyotiwa kimiyani na  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Danny Usengimana dakika ya 39, kabla ya Mshambuliaji Chipukizi Peter Paul aliyetokea benchi kuisawazishia Azam FC dakika ya 87.

No comments