TAHADHARI YA GUARDIOLA KWENYE KIKOSI CHA ENGLAND KINACHOELEKEA URUSI HII HAPA.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa anaamini timu ya taifa ya England itafaidika zaidi na wachezaji wanaocheza ligi tofauti nje ya EPL kwani wanakutana na aina mbalimbali za soka ambazo huwajenga. 


Kauli ya Guardiola imekuja katika kipindi ambacho England inajindaa na michuano ya Kombe la dunia nchini Urusi mwaka huu huku kikosi kikiwa kimesheheni wachezaji wanaocheza ligi ya EPL pekee.

"Nadhani kuhamia nchi nyingine na kucheza ligi zingine ni hatua nzuri ya kupata uzoefu mzuri na kuona hali tofauti na kuzoea aina tofauti ya mchezo kitu ambacho husaidia kwenye mashindano makubwa'', Guardiola.


England haijawahi kuwa na wachezaji wanaocheza nje ya EPL kwenye timu ya taifa tangu ifanye hivyo mwaka 2006 kwenye fainali za Kombe la dunia ambapo wachezaji David Beckham na Owen Hargreaves walikuwa wakicheza soka nje ya England.

Timu hiyo kwasasa ina wachezaji kadhaa ambao wanacheza ligi ya Bundesliga ambao ni mchezaji wa Everton Ademola Lookman aliyepo kwa mkopo kwenye timu ya RB Leipzig wakati mchezaji wa West Ham Reece Oxford naye yupo Borussia Monchengladbach kwa mkopo. 

Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.

No comments