TAIFA STARS KUSHUKA DIMBANI KESHO KUWAKARIBISHA CONGO KWENYE MCHEZO WA KIRAFIKI
Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kesho inashuka Dimba la Uwanja wa Taifa kuwakaribisha Timu ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki huku ikiwakosa wachezaji wawili akiwemo Mlinda Mlango Aishi Manula ambaye ni majeruhi.
Kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Hemed Moroco amesema, Kikosi chake kipo tayari kwaajili ya mchezo wa kesho isipokuwa watawakosa wachezaji wawili.
"Tunamajeruhi Makame na Aishi ambaye amepata tatizo la enda, wachezaji waliobakia naamini wapo tayari kupambana, hatuhitaji kupoteza mchezo huu, tutatumia kikosi kilekile cha Algeria kwasababu kipo vizuri katika kupambana, " amesema.
Kwaupande wake Kocha wa Dr Congo Ibenge Frolent amesema, anaamini utakuwa ni mchezo mzuri na kikosi chake anakiamini katika kupambana.
"Mchezo utakuwa ni mgumu, Taifa stars wamepoteza mchezo uliopita hivyo hawatakubali kupoteza tena na hakuna mchezo mwepesi nasisi pia hatutaki kupoteza mchezo huo kwahiyo nitatumia kikosi changu nilichokuja nacho ili kuhakikisha kinapambana na kinatoa matokeo mazuri, " amesema.
Kwaupande wake Nahodha msaidizi wa Timu hiyo Himid Mao amesema, an a amino kila mchezaji anajua nafasi yake na yoyote atakayepata nafasi atapambana kwaajili ya kuipa timu matokeo mazuri.
"Wachezaji wote tupo vizuri isipokuwa wachezaji wawili lakini naamini tuliobakia tutapambana ili kupata ushindi " amesema.
Naye Nahodha wa Dr Congo Benik Afobe amesema, wamekuja kwaajili ya kupambana na wachezaji wote wapo katika hali nzuri japo bado hajalijua soka laTanzania lakini watahakikisha wanapambana.
"Kiukweli sijalijua sana soka la Tanzania zaidi ya kuwajua baadhi ya wachezaji lakini tumejipanga kwaajili ya kupambana ili kuweza kuondoka na matokeo mazuri, " amesema.
Post a Comment