CHILUNDA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI MEI
Mshambuliaji wa timu ya Azam, Shaban Idd 'Chilunda' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi mwezi Mei.
Chilunda alifunga bao safi la tiktak katika mchezo wa mwisho wa kufungia msimu dhidi ya Yanga walioibuka na ushindi wa mabao 3-1 uliofanyika Mei 28.
Chilunda amechangia kwa kiasi kikubwa Azam kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi juu ya Yanga.
Mshambuliaji atakapewa pesa taslimu sh milioni moja, kisimbuzi cha Azam TV pamoja na Ngao.
Post a Comment