MASHABIKI WA SIMBA KUINGIA BURE KESHO FAINALI YA SPORTPESA
Uongozi wa klabu ya Simba umeweka utaratibu wa kuwalipia tiketi za kuingilia uwanjani mashabiki watakaosafiri kutoka nchini au sehemu nyingine kwa ajili ya fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup utakaopigwa kesho nchini Kenya.
Baadhi ya mashabiki wa mabingwa hao kutokana Tanzania wapo safarini kuelekea Kenya kwa ajili ya kuipa sapoti timu katika mchezo huo muhimu dhidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia.
Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Manara amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha mashabiki wengi wanajitokeza kwa wingi kuisapoti timu.
"Kila mshabiki atakayekuja kutoka nyumbani tutamlipia tiketi ya kuingilia uwanjani, tumeweka utaratibu mzuri na usalama umeimarishwa kikubwa tunahitaji kupata sapoti," alisema Manara.
Mchezo huo wa fainali utachezwa katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiri.
Safi sana chama letu Simba sc kwa kuona umuhimu wa fans wenu.
ReplyDeleteNa inshallah kesho Gor mahia anakufa haijalishi atafungwa kwa dk 90 au penati.
Kikubwa ni Simba sc kushinda hiyo game ya kesho.