STRAIKA MBENIN ATHIBITISHA YUPO MBIONI KUTUA YANGA



Mshambuliaji Marcellin Koukpo raia wa Benin amethibitisha yupo mbioni kujiunga na Yanga ambao wameonyesha nia ya kutaka kumsajili muda mrefu.

Kupitia akaunti ya Instagram ya klabu ya Yanga wameweka video ikimuonyesha mshambuliaji huyo akiwatakia asubuhi njema mashabiki wa Yanga.

Katika video hiyo Marcellin amewaahidi mashabiki wa Yanga kuwa muda si mrefu atakuja Tanzania kujiunga nao.

Usiku wa kuamkia leo msemaji wa klabu hiyo, Dismas Ten aliposti picha katika akaunti yake ya Instagram akiwa uwanja wa ndege pamoja na mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji huyo anachezea timu ya Buffles du Borgou ya Benin ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi hicho.

No comments