MBIVU, MBICHI MAJERAHA YA NGOMA KUJULIKANA KESHO
Uongozi wa klabu ya Azam umesema utaweka wazi juu ya majeraha yanayo msumbua mshambuliaji wao mpya Donald Ngoma kesho mbele ya Waandishi wa habari katika ofisi zao za Mzizima.
Ngoma pamoja na daktari wa timu hiyo Mwanandi Mwankemwa watawasili nchini usiku wa leo kutoka nchini Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya St. Vincent Parrot.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia Tiktaktza kuwa majibu ya vipimo vya mshambuliaji huyo yatawekwa hadharani mbele ya Wana habari kuanzia saa 6 mchana.
Jaffer ameongeza mbali na majibu ya vipimo vya Ngoma pia kesho watakuwa na mambo mengine yakiwemo masala ya usajili.
"Wadau wa soka wanataka kufahamu juu ya kinacho msumbua Ngoma na kesho tutakiweka wazi kama ataendelea kukaa nje au atarejea uwanjani na majeraha yake yapo kwenye hali gani," alisema Jaffer.
Azam wanahusishwa kupata saini ya mshambuliaji Ditram Nchimbi kutoka timu ya Njombe Mji ambapo huenda akatambulishwa hiyo kesho.
Post a Comment