RASMI KUTINYU ATUA AZAM FC
Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye klabu ya Azam imekamilisha usajili wa kiungo Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United.
Kupitia ukurasa wao Instagram, Azam imeweka picha ya kiungo huyo akiwa na meneja wao Philip Alando.
Singida wenyewe wameandika katika mtandao wa Instagram kuthibitisha usajili huo huku wakimtakia kila la kheri katika maisha yake ya mapya soka.
Kutinyu ameenguliwa katika kikosi cha wachezaji 20 cha Singida United kinachosafiri asubuhi hii kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza leo.
Kiungo huyo amemfuata kocha wake Hans van Pluijm ambaye alitangazwa wiki iliyopita kujiunga na matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.
Wawili hao walikuwa pamoja katika timu ya Singida msimu uliopita na jana walicheza mechi ya mwisho katika mchezo wa fainali ya FA waliolala mbele ya Mtibwa Sugar mabao 3-2.
Post a Comment