YANGA: MAKOSA YA KITOTO YAMETUTOA SPORTPESA SUPER CUP
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Yanga, Noel Mwandila amesema wachezaji wake walifanya makosa ya kitoto na kupelekea kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea nchini Kenya.
Yanga imekuwa ya kwanza kuaga michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kakamega Homeboyz katika mchezo wa ufunguzi.
Mwandila amesema walicheza chini ya kiwango na walistahili kutolewa kwenye michuano hiyo na wanaenda kujipanga kwa ajili ya mwakani.
Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji wake kadhaa walicheza wakitoka kuumwa huku wengine wakiukosa kutokana na kutokuwa fiti.
"Kilicho tutoa ni makosa ya kitoto waliyofanya wachezaji wangu, hatukucheza vizuri na tulistahili kutoka.
"Hatukuwa na msimu mzuri tumekutwa na misukosuko mingi lakini tunaenda kujiandaa kwa mashindano mengine," alisema Mwandila.
Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja Afraha mabao ya Kakamega yalifungwa na Allan Wanga aliyefunga mawili na Wycliff Opondo wakati lile la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Matheo Anthony.
Post a Comment